Tambua – Allaah akuwafikishe – ya kwamba hatua za maisha ni tano:

Ya kwanza: Kuanzia mtu anapozaliwa mpaka anapobaleghe ambako kunapitika pindi mtu anapofikisha miaka kumi na tano.

Ya pili: Kuanzia mtu anapobaleghe mpaka mwisho wa ujana wake, ambako kunapitika pindi mtu anapofikisha miaka thelathini na tano. Hii ndio miaka ya ujana.

Ya tatu: Kuanzia wakati huo mpaka pale mtu anapofikisha miaka khamsini. Kipindi hicho huitwa Kuhuulah.

Ya nne: Kuanzia miaka khamsini mpaka mtu anapofikisha miaka sabini. Hicho kipindi huitwa Shaykhuukhah.

Ya tano: Kuanzia miaka sabini mpaka mwisho wa uhai. Hiki ni kipindi kinachoitwa Haram.

Miaka tuliyoitaja inaweza kutofautiana. Ndio maana tumeigawa katika milango mitano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin al-Jawziy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyh-un-Naa’im al-Ghamr ´alaa Mawswim-il-´Umr, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 14/02/2017