01. Hadiyth “Kunaponadiwa kwa ajili ya swalah basi shaytwaan hugeuza mgongo… “

259 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إذا نوديَ بالصلاةِ أدبَرَ الشيطانُ وله ضُراطٌ؛ حتى لا يسمعَ التأذينَ، فإذا قُضِي الأذانُ أقبلَ، فإذا ثُوِّبَ أدبَرَ، فإذا قُضِيَ التثويبُ أقبلَ، حتى يخطُرَ بين المرءِ ونفسِه، يقولُ: اذكُرْ كذا، اذكر كذا، لِما لم يكنْ يَذْكُر من قَبلُ، حتى يَظَلَّ الرجلُ ما يدري كم صلّى

“Kunaponadiwa kwa ajili ya swalah basi shaytwaan hugeuza mgongo na huku akitoa pumzi ili asiweze kusikia adhaana. Adhaana inapomalizika basi husogea mbele. Pindi kunapokimiwa basi hugeuza mgongo. Kunapomalizwa kukimiwa basi husogea mbele mpaka akajipenyeza kati ya mtu na nafsi yake na akamwambia: “Kumbuka kitu fulani! Kumbuka kitu fulani!” Humfanya akayakumbuka mambo ambayo alikuwa hayakumbuki hapo kabla mpaka mwishowe akasahau ni kiasi gani ameswali.”[1]

Ameipokea Maalik, al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na an-Nasaa’iy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/223)
  • Imechapishwa: 09/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy