Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mwenye jukumu, Mwenye kutarajiwa kuitikia du´aa, Yeye ndiye ambaye tunaomba akupangilie mambo yenu mazuri duniani na Aakhirah, akumiminieni neema Zake za dhahiri na zilizojificha, akufanyeni muwe miongoni mwa wale ambao wanaponeemeshwa na Allaah, basi wanashukuru, wanapojaribiwa, basi wanavumilia na wanapotenda dhambi, basi wanaomba msamaha. Hakika mambo haya matatu ndiyo ufunguo wa furaha ya mja na alama ya ufanisi wake katika ulimwengu na Aakhirah. Hapana mja yeyote awezaye kuyaepuka, kwa sababu mja huwa daima yupo katika kupishana kati ya haya mambo matatu.
Neema kutoka kwa Allaah zinamiminika juu yake. Basi mfungamano wake ni kushukuru. Shukrani imejengwa juu ya nguzo tatu: kukubali neema hizo ndani kwa ndani, kuzitamka kwa nje na kuzitumia katika radhi ya Mmiliki wake, Mtoaji wake na Mwenye kuzimiminia. Basi akifanya hivyo, ameshukuru neema hizo japokuwa atakuwa amefanya upungufu katika ukamilifu wa shukrani.
Mitihani kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamjaribu nayo. Wajibu wake humo ni subira na kujiliwaza. Subira ni kuizuia nafsi kutolalamika juu ya yaliyompata, kuizuia ulimi kutokamana na malalamiko na kuizuia viungo kutofanya maasi kama vile kujigonga, kurarua nguo, kung´oa nywele na mfano wake. Basi msingi wa subira uko juu ya nguzo hizi tatu. Akizisimamia ipasavyo, basi msiba wake unageuka kuwa ni neema kwake, balaa linakuwa ni zawadi na kile ambacho hakipendezi kinakuwa kipenzi. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakumjaribu ili amwangamize; bali Amemjaribu ili ampime subira na utumwa wake. Kwa kuwa Allaah ana haki juu ya mja katika hali ya dhiki kama alivyo nayo katika hali ya raha. Lakini watu wengi wanaweza kufanyia kazi utumwa kwa kile wanachokipenda tu. Jambo kubwa ni katika kufanyia kazi utumwa katika mambo yasiyopendeza. Hapo ndipo daraja za waja zinatofautiana mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Mfano wa hayo ni kutawadha kwa maji baridi wakati wa joto kali ni uja. Kumkaribia mke wake mrembo ambaye anampenda pia ni uja. Kumgharamikia mkewe, yeye mwenyewe na familia yake ni uja. Hali kadhalika kutawadha kwa maji ya baridi wakati wa baridi kali ni uja. Kujiepusha na maasi ambayo nafsi yake inayatamani pasi na kuogopa watu ni uja. Kutumia mali katika hali ya dhiki ni uja. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya aina hizi mbili za uja. Hivyo basi anayekuwa mja wa Allaah katika hali zote mbili – ya kupendeza na ya kuchukiza – akiwa anasimama kwa haki ya Allaah katika hali ya furaha na ya dhiki, huyo ndiye aliyekusudiwa katika maneno ya Allaah:
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِكَافٍ عَبْ
”Je, kwani Allaah si Mwenye kumtosheleza mja Wake?”[1]
Imekuja katika kisomo kingine ”waja Wake” (عباده). Maana zote mbili ni sawa, kwa sababu neno la umoja likiwa limeambatanishwa hujumlisha maana ya wingi. Kwa hiyo ulinzi kamili uko pal-Waabil as-Swayyibamoja na utumwa kamili na ule wa upungufu. Basi yule aliyekuta kheri na amshukuru Allaah, na yule aliyekuta kinyume cha hivyo basi asijilaumu isipokuwa nafsi yake mwenyewe.
[1] 39:36
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 5-7
- Imechapishwa: 27/07/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 5-7
Imechapishwa: 27/07/2025
https://firqatunnajia.com/01-funguo-tatu-za-furaha-na-mafanikio-ya-milele/