Shaykh Bakr Abu Zayd amesema:

“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemewa.

Muheshimiwa na Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy

as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh

Nimerejesha matakwa yako juu ya kusoma kitabu kilichoambatanishwa “Adhwaa´ Islaamiyyah ´alaa ´Aqiydati Sayyid Qutwub wa Fikrih” ili kupata makosa. Je, makosa haya yatazuia mchakato ili kisichapishwe? Au kuna uwezekano yakarekebishwa ili kichapishwe na kisambazwe ili ulipwe thawabu Aakhirah na waja Wake wapate uelewa hapa duniani? Kwa hiyo naanza kwa njia hii… “[1]

Nimetuma kitabu kwa wanachuoni wengi akiwemo muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn, Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan, Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad, Shaykh Muhammad bin Amaan al-Jaamiy, Shaykh Zayd bin Muhammad Haadiy al-Madkhaliy, Shaykh Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy na Shaykh Bakr Abu Zayd kwa kutaraji wanionyesha makosa yangu kama kweli yapo kwa vile watu wote hukosea isipokuwa Mitume na Manabii (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) waliokingwa na kukosea. Sikumwomba yeyote katika wao kukizuia kitabu hichi kilichobarikiwa ambacho kiko mahiri – na himdi zote ni za Allaah – kwa kuinusuru haki na kuiponda batili.

[1] Uk. 01