Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah kwa uumbaji, uendeshaji, kumtakasia Yeye ´ibaadah, kuacha kuabudu vyenginevyo, kuacha kuabudu wengine asiyekuwa Yeye, kumthibitishia majina Yake mazuri mno na sifa Zake tukufu na kumtakasa kutokamana na mapungufu na kasoro. Maana hii imekusanya ndani yake aina tatu za Tawhiyd. Ubainifu wake ni ifuatavyo:

1- Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Ndani yake kuna sura zifuatazo:

Sura ya kwanza: Ubainifu wa maana ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, maumbile yake na kwamba washirikina walikuwa wakiikubali.

Sura ya pili: Ufahamu wa neno ´Mola` ndani ya Qur-aan na Sunnah na mitazamo ya nyumati zilizopotea katika mlango wa uola na kuiraddi mitazamo hiyo.

Sura ya tatu: Ubainifu wa unyenyekeaji wa ulimwengu katika ujisalimishaji na kumtii Allaah.

Sura ya nne: Ubainifu wa mfumo wa Qur-aan katika kuthibitisha upwekekaji wa Allaah katika uumbaji, riziki na mengineyo.

Sura ya tano: Ubainifu wa kwamba Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah inapelekea Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 22/01/2020