Zip kwenye mavazi ya mwanamke II


Swali: Inasemekana kwamba zip inayowekwa na wanawake katika mavazi yao kwa nyuma ni haramu na kadhalika mavazi yenye kubana, sidiria za matiti na rangi nyekundu ya mdomo. Tunaomba utupe faida.

Jibu: Zip zinazokuwa nyuma kwa wanawake tunaona kuwa hazina neno na hazina ubaya. Msingi katika mavazi, aina na namna, ni uhalali. Isipokuwa yale yaliyotajwa na dalili juu ya uharamu wake. Hapana shaka kwamba kilichozoeleka kuanzia wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), zama zengine mpaka katika zama zetu hizi ni kwamba mfuko unakuwa kwa mbele na hauwi nyuma. Lakini kusema kwamba mtu akienda kinyume na ada hii amefanya haramu au jambo lenye kuchukizwa ni kitu kisichowezekana isipokuwa kwa dalili kutoka katika Shari´ah. Kukija dalili kutoka katika Shari´ah inayosema kuwa jambo hili limechukizwa basi tutaitendea kazi. Vinginevyo msingi ni kuruhusu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6811
  • Imechapishwa: 13/03/2021