Zakaat-ul-Fitwr ataitoa katika nchi gani?

Swali: Nusu moja ya Ramadhaan nitakuwa Saudia na nusu nyingine nitakuwa katika nchi yangu. Zakaat-ul-Fitwr nitaitoa lini?

Jibu: Ataitoa usiku wa kuamkia idi na kabla ya kwenda kuswali idi. Mahali popote; ni mamoja kama atakuwa Saudia au katika nchi yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2vQdgZLzLuI
  • Imechapishwa: 12/05/2020