Zakaah kwa ajili ya kutengeneza barabara


Swali: Inajuzu kutoa zakaah kwa ajili ya kutengeneza kazi ya barabara ya kijiji ambayo haiwezi kufanywa kwa njia nyingine?

Jibu: Hapana. Zakaah haitolewi kwa ajili ya barabara wala miradi ya kijumla. Inatolewa kwa ajili ya wale watu aina saba waliotajwa katika Aayah:

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗوَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

“Hakika zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [ili kuingia katika Uislamu] na kuwakomboa watumwa na [kuwasaidia] wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri – ni faradhi itokayo kwa Allaah. Na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (09:60)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2017