Yule ambaye ana kitu cha kumwambia mtawala


Swali: Ni ipi hukumu ya kuwakemea watawala juu ya mimbari wakati wa Khutbah ya ijumaa na kwenginepo?

Jibu: Huku ni kuasi na ni kujivua katika utiifu wa mtawala kwa maneno. Uasi unaweza kuwa kwa silaha kama ambavyo vilevile unaweza kuwa kwa maneno hata kama mtu hakubeba silaha. Haijuzu kufanya hivi. Watawala wa waislamu wanatakiwa kuombewa du´aa  ya mafanikio na wepesi. Watawala wengine sisi hawatuhusu. Ama watawala wa waislamu haifai kuwakataza hadharani. Ikiwa uko na nasaha basi unachotakiwa ni wewe kufanya kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye anataka kumnasihi mtawala basi asifanye hivo hadharani. Badala yake anatakiwa kumshika mkono na kuwa nae faragha. Ima apokee kutoka kwake au ameshatekeleza wajibu wake.”[1]

Watawala wana heshima zao. Haitakiwi kuwaponda na kuwakaripia hadharani.

[1] Ibn Abiy ´Aaswim (1097). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 17/12/2017