al-Fadhwl amesema:

“Alifikiwa na khabari – Ahmad – juu ya mtu anayesema: “Allaah hatoonekana siku ya Qiyaamah.” Akasema: “Allaah amlaani! Yeye yuko katika watu gani? Je, Allaah si ndiye kasema:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَى رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

“Kuna nyuso siku hiyo zitang´ara – zikimtazama Mola wao.”[1]

pia:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Sivyo hivyo. Bali wao siku hiyo watazuiwa kumuona Mola wao.”[2]?

al-Fadhwl akasema:

“Nimemsikia Ahmad bin Hanbal akisema: “Watu waongo kabisa ni waombaji na wapiga visa.”

[1] 75:22-23

[2] 83:15

  • Mhusika: Imaam Abuul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/193)
  • Imechapishwa: 10/06/2017