Yasipotimia haya haijuzu haijuzu kumg´oa mtawala kafiri

Swali 07: Iwapo tutakadiria kwamba kuna uasi unaokubalika Kishari´ah kwenye kundi miongoni mwa makundi. Je, jambo hili litatakasa kuwaua wale wasaidizi wa mtawala huyu na kila ambaye anafanya kazi serikalini kama mfano wa polisi, wenye kuchunga amani na wengineo?

Jibu: Nimeshatangulia kukujuza kwamba haijuzu kufanya uasi kwa mtawala isipokuwa kwa kutumia masharti mawili:

1- Kuwepo na ukafiri wa wazi ambao una ushahidi kutoka kwa Allaah.

2- Uwezo wa kumg´oa mtawala ung´oaji usiopelekea katika shari kubwa kuliko. Yasipotimia hayo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdu-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 111
  • Imechapishwa: 20/12/2019