Wudhuu´ wa mwanamke mwenye utoko wenye kuendelea

Swali 321: Anapotawadha mwanamke anayetokwa na utoko wenye kuendelea kwa ajili ya swalah ya faradhi – je, inafaa kwake kuswali swalah ya Sunnah na kusoma Qur-aan kwa wudhuu´ wa faradhi hiyo mpaka kutapoingia faradhi ya pili?

Jibu: Akitawadha kwa ajili ya kuswali swalah ya faradhi mwanzoni mwa wakati basi inafaa kwake kuswali atakayo katika swalah za faradhi na za Sunnah na kusoma Qur-aan mpaka pale kutapoingia wakati wa swalah nyingine.

Swali 322: Inasihi kwa mwanamke huyo kuswali swalah ya Dhuhaa´ kwa wudhuu´ wa Fajr?

Jibu: Si sahihi kufanya hivo. Swalah ya Dhuhaa´ imepangiwa muda maalum. Ni lazima kutawadha kwa ajili yake baada ya kuingia wakati wake. Kwa sababu mwanamke huyo ni kama mwanamke mwenye kutokwa na damu ya ugonjwa. Mtuume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwamrisha mwanamke mwenye kutokwa na damu ya ugonjwa kutawadha kwa ajili ya kila swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 121
  • Imechapishwa: 02/10/2019