Wudhuu´ wa mwanamke anayetokwa na utoko na istihaadhah

Swali: Kuhusu utoke unaomtoka mwanamke, mwanamke afanye nini pindi anapotawadha? Je, aswali faradhi moja kwa moja au aswali kwanza Sunnah na hivyo hali yake iwe kama ambaye hakutokwa na kitu?

Jibu: Mwanamke mwenye kutokwa na damu ya ugonjwa au mwanamke ambaye anatokwa na majimaji siku zote anapoingiliwa na wakati wa swalah anatakiwa kutawadha. Atabaki na wudhuu´ wake mpaka wakati utoke. Katika hali hiyo ataswali swalah za faradhi na za sunnah anazotaka kwa sababu twahara yake ni timilifu japokuwa ni twahara ya dharurah inayotakiwa kukadiriwa kiasi cha kiwango chake. Ni twahara inayotakiwa kukadiriwa kiasi cha kiwango chake namaanisha kwamba wakati wa swalah ukitoka anatakiwa basi atahitajia kutawadha kwa mara nyingine kwa ajili ya kuswali swalah zilizoko huko mbele.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/692
  • Imechapishwa: 25/10/2017