Wewe ni jina la Allaah?


Swali: Wewe ni jina miongoni mwa Majina ya Allaah na mtu akawa anaomba kwalo kwa kusema “Ee wewe! Niruzuku” na kadhalika?

Jibu: Hakuna mwanachuoni yeyote aliyesema hivi. Suufiyyah ndio husema “Huu!”, “Huu!”, “Huu!” au “Allaah!”, “Allaah!”, “Allaah!”. Haya ni mambo ya Suufiyyah. Bali haya ni mabaya zaidi kuliko wanayofanya Suufiyyah. Suufiyyah husema hivi kama dhamiri ya Allaah. Ama wewe haina dhamiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_04.mp3
  • Imechapishwa: 01/07/2018