Wenye kukhasirika walojigonga kwenye jibali

Siku moja nilisoma makala katika gazeti la “al-Bayaan” au “as-Sunnah”, ambapo Shaykh al-Albaaniy alikuwa amevamiwa. Baadhi ya kurasa akawa anasifiwa Shaykh Ibn Baaz. Wamefanya hivyo ili mtu asije kusema ya kwamba wanawatukana wanachuoni. Wakati Shaykh Ibn Baaz (Hafidhwahu Allaah) alipotoa fatwa kwamba inajuzu kufanya mkataba wa amani na mayahudi wakazuka na wakawatuhumu wanachuoni kuwa ni wajinga. Wakawatuhumu kwa tuhumu chafu.

Wewe ni nani, Muhammad Suruur, nyiyni ni kina nani, wafuasi wake, kwa kujigonga kwenye jibali na kuwatukana wanachuoni wakubwa? Nyinyi ni kipote kilichokhasirika! Sasa watu wamejua nyinyi ni kina nani. Suruuriyyah na wafuasi wa ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq ni mlango uliofunguliwa kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=21
  • Imechapishwa: 14/07/2020