Swali: Sisi tuko na mtu Suufiy ambaye huwaandikia makaratasi wanawake na anawaamrisha waziweke ratasi hizo vichwani mwa watoto wao. Karatasi hizi zinaitwa ´Bakkaaya`. Huandika vilevile Aayah, mashairi na du´aa mbalimbali zisizoafikiana na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni ipi hukumu ya makaratasi haya na du´aa hizi?

Jibu: Ndio, wako makhurafi wenye ´Aqiydah mbovu ambao wanawatibu watu kwa mambo ya kishirki, hirizi, herufi za mkato na majina ya mashaytwaan. Wanayaandika haya na wanawapa watu kwa aina ya hirizi. Ni wajibu kutahadhari na haya. Huku ni kumshirikisha Allaah (Ta´ala). Huku ni kutundika hirizi. Hii ni hirizi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutundika hirizi basi ameshirikisha.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Mwenye kutundika hirizi basi Allaah atamwegemeza nayo.”

“Hakika matabano, at-Tiwalah na hirizi ni shirki.”

Haijuzu kuridhia mambo haya, kuyafanyia kazi au kuzipokea hirizi hizi. Mimi nimeshakwambieni kwa mtu asende kutibiwa isipokuwa kwa aliye na ´Aqiydah [sahihi], dini na maarifa[1]. Wanachuoni wahakiki hawawaandikii watu hirizi. Wenye kufanya haya ima ni wajinga au makhurafi. Kwa hiyo kitendo hichi hakifai kabisa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/usende-kwa-msomaji-ruqyah-asiyetambulika/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 04/01/2019