Waume wanaowakataza wake zao kuolewa baada ya kufa

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kujizuia kuolewa baada ya kufiliwa na mume wake wa kwanza au mwanamume akamuamrisha mke wake asiolewe na mwanaume mwingine endapo yeye atakufa kabla yake?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kujizuia kuolewa baada ya kufiliwa na mume wake. Hayo ni mambo maalum kwa wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake.

Vilevile haijuzu kwa mwanaume kumkataza mke wake kuolewa baada ya yeye kufa na wala haimlazimu mwanamke kumtii katika hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika utiifu unakuwa katika mambo mema.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7145), Muslim (1840), an-Nasaa´iy (4205) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/18)
  • Imechapishwa: 04/08/2017