4Yule mtu akanipeleka mbele ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, kwa njia ya lango la kaskazini. Nilipoangalia, nikaona utukufu wa Mwenyezi Mungu umeijaza nyumba ya Mwenyezi Mungu. Hapo nikaanguka kifudifudi. 5Mwenyezi Mungu akaniambia: “Wewe mtu! Tia maanani mambo yote unayoona na kusikia. Nitakueleza kanuni na masharti ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. Zingatia moyoni mwako kwa makini, ni watu gani wanaoruhusiwa kuingia na kutoka katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na ni watu gani wamekatazwa kuingia humo.

6Utawaambia hao watu waasi wa israeli, Bwana Mwenyezi Mungu asema hivi: “Siwezi kuendelea kuyavumilia machukizo yenu yote. 7Mmeitia unajisi maskani yangu kwa kuruhusu waingie humo watu wasiotahiriwa, watu wasionitii mimi, wakati mafuta na damu vinatambikwa kwa ajili yangu. Hivyo, nyinyi watu wangu mmelivunja agano langu kwa machukizo yenu yote. 8Badala ya kutekeleza huduma ya vitu vyangu vitakatifu, mmeruhusu watu wa mataifa mengine kutekeleza huduma hiyo katika maskani yangu. 9Sasa, mimi Bwana Mwenyezi Mungu nasema hivi: “Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ezekieli 44:04
  • Imechapishwa: 28/01/2020