Watoto wanatakiwa wafanyiwe ukali katika jambo la swalah kukiwemo Fajr

Swali: Mtoto ambaye miaka yake ni kati ya saba mpaka kumi afanyiwe mkazo inapokuja katika masuala ya swalah au apelekwe polepole?

Jibu: Hapana, asipelekwe polepole. Wapigeni watapofikisha miaka kumi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wapigeni kwayo watapofikisha miaka kumi.”

Swali: Je, nimwamshe kwa ajili ya kuswali Fajr katika mkusanyiko au ni sawa kumwamsha mpaka pale wakati atakapoenda masomoni?

Jibu: Hapana, haijuzu kumwacha na akaichelewesha. Ni lazima kwake kuamka na aswali pamoja na waislamu wenzake. Kisha baada ya kumaliza kuswali arudi kulala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2019