Swali: Je, ni sahihi kwamba picha zilizoharamishwa ni zile za kiwiliwili na si zile za kuchorwa au za kivuli?

Jibu: Hapana. Hili ni kosa na si sahihi. Picha zote ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengenezaji picha, pasi na kumvua yeyote katika wao. Amewalaani watengenezaji picha kwa ujumla, ni mamoja ni kwa kuchonga, kuchora kwa mkono au kwa kutumia vifaa vya kisasa. Hadiyth ni zenye kuenea na laana ni yenye kuenea. Ni nani ambaye anataka kubagua kile kilichofanywa kuenea na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema kuwa jambo hili ni lenye kufaa na lingine ndio haramu?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (93) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighstah%20-20-1-1440_0.mp3
  • Imechapishwa: 12/04/2019