Watatoka Motoni pasi na kufanya matendo mema hata siku moja

Swali: Ni vipi tutaielewa Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) isemayo:

“Malaika wameombea, Mitume wameombea, waumini wameombea na aliyebaki ni Mwingi wa wenye huruma.” Halafu Allaah atawatoa ndani ya Moto watu ambao hawajapatapo kufanya kheri hata siku moja.”[1]?

Jibu: Tutaifahamu kwamba ni yenye kuenea na dalili zinazomkufurisha asiyeswali ni maalum. Ni jambo lenye kutambulika kwa wanachuoni kwamba dalili zilizoenea zinafanywa maalum na zile dalili ambazo ni maalum. Hadiyth haikutaja mtu ambaye alikuwa haswali mpaka tuseme kwamba inapingana na dalili zinazojulisha ukafiri wa ambaye haswali. Amesema kwamba hakuwahi kufanya kheri hata siku moja. Swalah haikutajwa, Hadiyth imekuja kwa ujumla. Dalili zinazofahamisha kwamba asiyeswali ni kafiri ni maalum na hivyo zile zilizokuja kwa ujumla zinafanywa maalum na zile ambazo ni maalum.

[1] al-Bukhaariy (7439) na Muslim (183).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-As-ilah al-Qatwariyyah, uk. 14-16
  • Imechapishwa: 03/02/2019