Wasikilizaji siku ya ijumaa hawaelewi kiarabu


Swali: Ikiwa wasikilizaji hawaelewi na wala hawajui lugha ya kiarabu. Je, inajuzu kwa Khatwiyb kuwatolea Khutbah kwa lugha yao?

Jibu: Ndio. Ikiwa hawafahamu lugha ya kiarabu awazungumzishe kwa lugha yao wanayoielewa.

Swali: Ikiwa katika wao kuna ambao wanajua lugha ya kiarabu na wengine hawajui. Je, awatolee Khutbah mara mbili; moja kwa kiarabu…

Jibu: Hapana. Awatolee Khutbah moja na wakati huohuo anawafasiri. Anaongea baadhi ya maneno na huku anayafasiri au anatoa Khutbah yote kwa kiarabu na imamu akishatoa Tasliym wafasiriwe kwa lugha yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017