Wanawake kuoneshana ´Awrah zao


Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kumuonesha baadhi ya ´Awrah yake mwanamke mwenzake?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi, sawa kwa mwanamke au mwanaume. Isipokuwa ikiwa ameenda kutibiwa kwa daktari mwanaume na akalazimika kuonesha kitu katika ´Awrah yake kwa ajili ya matibabu, katika hali hii hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014