Wanasoma Takbiyr za swalah ya ´iyd kwa sauti ya juu

Swali: Maamuma wananyanyua sauti ya juu katika zile Takbiyr zenye kuzidi. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno. Lakini hata hivyo wasinyanyue sauti juu sana. Inatakiwa iwe kwa kiwango cha kuweza kujisikia wao wenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 02/06/2019