Wanaocha kulingania Salafiyyah kwa kuogopa watu ni kupendelea dunia kuliko Aakhirah


Swali: Sisi tunapenda kuwa katika walinganizi wa mfumo wa Salaf na kuueneza. Lakini pindi tunapokabiliwa na unyanyasaji katika kazi na masomo yetu tunalazimika kunyamaza na kusubiri juu ya unyanyasaji. Ni zipi nasaha zako juu ya hayo?

Jibu: Ni lazima kwa watu hawa wawe na subira, wawe imara na wazungumze haki kwa hekima na kwa dalili. Wasiogope juu ya Allaah lawama za wenye kulaumu. Wasiogope juu ya kazi. Hii ni moja ya mitego ya shaywaan:

إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki wake. Hivyo basi msiwakhofu na mnikhofu Mimi mkiwa kweli ni waumini.”[1]

Kwa hali yoyote yule ambaye anaficha haki kwa sababu ya kuchelea kazi yake naona kuwa amependekeza dunia kuliko Aakhirah. Lau kila mtu angelikuwa anafanya hivi na khaswa katika nchi kama hii ambayo uwanja ni mpana sana na hakuna yeyote kamwe awezaye kukuzuia na kazi. Huku ni kuogofya kwa shaytwaan. Ni wajibu kwa mtu huyu amche Allaah na wala asimwogopi shaytwaan.

[1] 03:175

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: Asbaab-un-Inhiraaf wat-Tawjiyhaat Manhajiyyah http://rabee.net/ar/questions.php?cat=27&id=200
  • Imechapishwa: 28/04/2018