Walii wa kweli hafanyi haya mbele za watu

Swali: Ambaye atadhihirisha na kufanya mambo yasiyokuwa ya kawaida mbele ya umati tuhukumu kuwa ni katika mawalii wa Allaah? Je, inajuzu kwetu kuomba ponyo kutoka kwake kwa idhini ya Allaah?

Jibu: Kuhukumu kuwa ni walii wa Allaah kwa sababu tu amefanya jambo lisilokuwa la kawaida si sahihi. Ni lazima kwanza kutazama matendo yake. Ni kweli kwamba itakuwa ni karama iwapo matendo yake ni mema na ´Aqiydah yake ni sahihi.

Lakini walii wa kihakika hadhihirishi mambo haya mbele ya watu. Badala yake humnyenyekea Allaah. Walii wa kihakika haingiwi na kiburi na kujiona kwa sababu ya karama hizi. Kinyume chake hujitahidi huzificha kadri na anavyoweza na hazidhihirishi mbele ya watu. Endapo atafanya hivo huashiriwa kidole. Lakini kwa hali yoyote tazama matendo yake na yale anayofuata. Katika hali hiyo ima atakuwa ni walii wa Allaah kweli na hivyo [ayafanyayo] itakuwa ni karama au akawa ni adui wa Allaah na hivyo [ayafanyayo] itakuwa ni mambo ya kishaytwaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 06/10/2016