Swali: Ni ipi tafsiri ya Maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

“Sema: “Je, Tukujuze ju ya wale waliokhasirika mno kwa matendo? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika maisha ya dunia na huku wao wakidhani kuwa wanapata mazuri kwa matendo yao.” (18:103-104

Jibu: Allaah amebainsha ni wepi; ni wale waliopoteza nguvu zao katika dunia hii na huku wanadhani kuwa wanafanya vyema. Ni makafiri, washirikina na wazushi. Wanaguswa na Aayah hii. Wanadhani kuwa matendo yao ni mema ilihali matendo yao ni batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (70) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%20-%2019%20-0%207%20-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 14/09/2018