6Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema: “Usioe mke katika binti za Wakanaani”, 7tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu. 8Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani. 9Ndipo Esau akaenda kwa Ismaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ismaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mwanzo 28:06-09
  • Imechapishwa: 14/01/2020