Wakati wa kusoma Adhkaar za jioni

Swali: Lini zinasomwa Adhkaar za jioni? Je, ni baada ya ´Aswr au Maghrib?

Jibu: Ni baada ya ´Aswr. Kama alivosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika “al-Waabil as-Swayyib” na akatumia dalili kwa maneno Yake (Ta´ala):

فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا

“Basi subiri juu ya yale wanayoyasema na tukuza kwa himdi za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla kuzama kwake.”[1]

Kabla ya kuzama kwa jua ni baada ya ´Aswr mpaka wakati wa kuzama kwake. Kadhalika baada ya Fajr mpaka wakati wa kuzama kwa jua. Wapo baadhi yao ambao wameonelea kwamba ni baada ya Maghrib. Wapo wengine ambao wameonelea kwamba jambo hili kuna wasaa ndani yake na kwamba inakuwa baada ya ´Aswr na baada ya Maghrib. Lakini bora zaidi ni baada ya ´Aswr na baaa ya Fajr. Ikiwezekana basi hili ndilo bora zaidi mpaka wakati wa kuzama kwa jua mpaka wakati wa kuchomoza kwake. Mtu akisoma Adhkaar za jioni baada ya Maghrib hakuna neno ikiwa ndio nafasi aliyopata.

[1] 20:130

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2018