Wakati umefika wa kurudi nyumbani badala ya kupiga kura

Swali: Ni ipi hukumu ya wale waislamu wachache kupiga kura katika miji ya kikafiri?

Jibu: Mosi haijuzu kwako kuishi katika miji ya makafiri na chini ya utawala wa makafiri isipokuwa kwa dharurah:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖوَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلً فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao, watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni [Moto wa] Jahannam – na uovu ulioje mahali pa kuishia. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah Akawasamehe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria.” (04:97-99)

Waishi kwa kiwango tu cha ile dharurah. Lakini wasiingie ndani ya mambo ya hukumu, kupiga kura na mfano wake. Wasijiingize ndani ya mambo haya. Kwa sababu katika hali hiyo watamchagua kafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=pqY0n63pMWE&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 18/10/2020