Swali: Tunawaona vijana wengi waliopewa mtihani wa Takfiyr na hakuna waliosalimika isipokuwa wale waliorehemewa na Mola.

al-Albaaniy: Kweli.

Swali: Unasemaje juu ya yule ambaye hatofautishi maneno ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu kufuru ndogo, Kufr dunaa Kufr, katika maudhui haya na bali anajaribu kuyaondosha kabisa kutoka kwa Salaf?

Jibu: Nasema kuwa mtu huyo ni mjinga au anafanya kuwa mjinga. Allaah ndiye atamtosheleza. Ni kipi zaidi tunaweza kusema juu yake? Mmepata kaseti inayowaraddi watu hawa. Kuhusu kile ninachosema juu yao tayari mmekwishakijua hivi sasa.

  • Mhusika: Imâm Muhammad Nâsir-ud-Dîn al-Albânî
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (915) Tarehe: 1417-03-20/1996-08-05
  • Imechapishwa: 07/06/2021