Waalimu wa kike kwenda sehemu ya 90 km bila Mahram

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuteua mwalimu wa kike ambaye atasafiri pamoja na waalimu wa kike wenzake wakiongozwa na dereva wa kiume ambaye ni ajinabi kwao na wakati huohuo wakawa hawana Mahram. Je, inajuzu kufanya hivo?

Jibu: Naona kuwa hakuna ubaya kufanya hivo. Mwanamke akiteuliwa katika nchi ambayo si yake aende huko kila siku na kurudi siku hiyohiyo akiwa pamoja na marafiki zake na kusitokee dereva na mwanamke kukaa faragha, hakuna ubaya. Hii haizingatiwi kuwa ni safari. Haijalishi kitu hata kama itafika 80 km au 90 km na wao wanarudi siku hiyohiyo, hii sio safari. Kwa hivyo hawahitajii kuwa na Mahram. Lakini kilichokatazwa ni wao kukaa faragha; dereva kukaa faragha na mmoja katika wao. Haijali kitu hata kama watakuwa ndani ya mji. Kwa sababu kuwa faragha pamoja na dereva ni haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1318
  • Imechapishwa: 27/10/2019