Swali: Unasemaje juu ya vitabu vya Ahl-us-Sunnah vilivyokaguliwa na Hizbiyyuun?

Jibu: Naona kuwa vitabu vinavyokaguliwa na Hizbiyyuun wanavitumia vibaya. Wanalainisha mipaka katika vitabu hivyo mpaka ionekane kuwa mwandishi anaongelea jambo maalum na suala maalum. Malengo ya mwandishi kwa kitabu hicho ni kuwakinaisha waislamu kwa kutumia Qur-aan, Sunnah na uelewa wa Salaf, ambapo Hizbiy aliyeungua anajaribu kufanya ionekane kwa njia nyingine na kuwapoteza watu na malengo ya mtunzi. Vitabu vya zamani vinahitajia kuwa vimesalimika na matamanio, mikono misafi na fikira zilizosalimika ivitumikie na kuvieneza ili kuyalinda maandiko yake, maana yake na malengo yake.

Hapo kale Ashaa´irah na Suufiyyah walikuwa wanaweza kuvitumia vibaya vitabu vya Hadiyth na tafsiri za Qur-aan na kuvipindisha kwa njia inayoendana nao. Vivyo hivyo ndivyo wanavyofanya wahakiki waliokuja nyuma. Kwa mfano al-Kawthariy. Alikuwa anaweza kutumia vibaya malengo ya kitabu na kukipindisha kikamilifu. Hali kadhalika ndivyo anavyofanya Hizbiy anayechukua kitabu na kukipindisha kwa njia inayolingana na mfumo wake na kadhalika. Hii ni khiyana na kielimu. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwa Ahl-us-Sunnah wafanye bidii ya kutumikia mirathi ya Salaf. Watu hawa wakiwahi kabla na kuvitumia vibaya vitabu basi Ahl-us-Sunnah wanatakiwa kuvisahihisha. Wanatakiwa wavikague upya, kuvisahihisha, kuvikagua sahihi na waweke wazi maana yavyo kwa mujibu wa mfumo wa Salaf.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf-us-Sittaar, uk. 24
  • Imechapishwa: 29/01/2017