Swali: Vipi imani itakuwa imara na kuihesabu katika mwezi wa Ramadhaan?

Jibu: Imani inazidi kwa kukithiri ´amali njema,  akaswali, funga, visimamo, akakumbusha, akalingania, akatoa swadaqah akafanya istighfaar – imani inazidi. Ama kuhusu kuifanyia hesabu ni juu yake kupigana Jihaad na nafsi yake kwa hesabu, yaani akawa anafanya ´amali kwa kutotaka pato lolote katika mambo ya kidunia, anataka kwa ´amali hizo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاء رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake basi na atende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ´ibaadah ya Mola wake.” (18:110)

Anayetaka katika ´amali azifanyazo Allah pamoja na jengine, basi kashirikisha katika ´Ibaadah ya Mola wake. Fanya ´amali usitake jengine ila Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah akulipe kwazo, akutakabalie, ajaalie ikawa ni sababu ya kuokoka kwako na Moto. Tunamuomba Allaah Ikhlaasw katika maneno na vitendo vyetu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020