Swali: Imethibiti kwamba Allaah hushuka katika theluthi ya mwisho ya usiku kwa njia inayolingana na utukufu na ukubwa Wake. Theluthi ya mwisho ya usiku inatofautiana kutoka sehemu hadi nyingine. Inakuwa vipi?

Jbu: Mtu huyu anauliza ifuatavyo: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (Tabaarak wa Ta´ala) huteremka katika mbingu ya dunia pindi kunapobakia theluthi ya mwisho ya usiku na kusema: “Ni nani anayeniomba nimjibie? Ni nani anayeniuliza nimpe? Ni nani anayenitaka msamaha nimsamehe? Huendelea hivi mpaka alfajiri iingie.””

Theluthi ya mwisho ya usiku ndio Allaah hushuka. Sehemu yoyote katika ardhi ulipo inapofika theluthi ya mwisho ya usiku ndio kipindi ambacho Allaah hushuka.

Kuhusiana na kwamba inatofautiana kutoka sehemu hadi nyingine inatokamana na kwamba muulizaji amefananisha sifa za Allaah na sifa za viumbe, kushuka kwa Muumba na kushuka kwa viumbe. Utatizi kama huu unaoulizia unauliziwa juu ya kiumbe. Ama Muumba hatujui namna anavyoshuka. Kushuka ni kitendo anachokifanya na wakati huo huo yuko juu ya ´Arshi (Subhaanahu wa Ta´ala). Inapofika theluthi ya mwisho ya usiku popote ulipo katika ardhi ndio wakati Allaah hushuka. Kuhusu inakuwa namna gani usitafiti hilo na kusema inatofautiana kutoka sehemu hadi nyingine. Hili ni gumu kwa kiumbe. Inapokuja kwa Muumba haistahiki kuuliza swali kama hili.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu akijibu swali hili kwa jina “Sharh Hadiyth-in-Nuzuul” ambapo walizozana watu wawili mmoja wao alisema usiku unatofautiana kutoka sehemu hadi nyingine.

  • Mhusika: ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah (01)
  • Imechapishwa: 01/05/2020