Vikao vingi vya wanawake


Swali: Katika vikao vyetu wanawake mazungumzo ya kufitinisha yanakuwa mengi kati yetu. Lakini wanawake wengi wanawazungumzia wengine. Je, kufanya hivo ni kueneza uvumi na usengenyi? Unawanasihi nini?

Jibu: Kujishughulisha katika kuzikiuka heshima za watu, kuwaponda, kuwatukana na kupeleleza kasoro zao si jambo la sawa. Dada zako wa kiislamu unatakiwa kuwapenda kwa ajili ya Allaah. Ukiona kosa kwa dada yako mnasihi kati yako wewe na yeye tu. Lakini kuzungumzia kwenye vikao aibu za watu ni kitu kinacholeta chuki na kutengana. Ni usengenyi uliokatazwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-13-11-1435هـ-0
  • Imechapishwa: 19/06/2022