Video camera harakati za wanafunzi na kuzitawanya

Swali: Masomoni kunafanyika harakati mbalimbali kukiwemo nad-wah, mihadhara na harakati nyenginezo zinazowanufaisha wanafunzi. Je, inajuzu kuchukua video camera harakati hizi na kuzihifadhi kwa ajili ya masomo au ili wanafunzi waweze kufaidika nazo?

Jibu: Ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa ni sawa zikachukuliwa harakati hizi kwa video camera ili ziweze kubaki na watu waweze kufaidika nazo baadae.

Ama yakiwa hayana faida basi itambulike kuwa ni kupoteza pesa na wakati.

Yakiwa yana faida lakini hata hivyo madhara yakawa ni makubwa kuliko faida, kama kwa mfano kukachukuliwa video matukio ambayo katika kuyatazama ndani yake kuna fitina, katika hali hii ni jambo linatakiwa kukatazwa.

Kwa kifupi ndani yake kukiwa kuna manufaa ni sawa. Vinginevyo itakuwa ni kupoteza pesa na wakati.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1011
  • Imechapishwa: 09/02/2019