Viatu vyenye kisigino kirefu


Swali: Ni ipi hukumu ya Uislamu kuhusu kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu?

Jibu: Angalau kwa uchache kabisa ni kitu kilichochukizwa. Mosi vina udhanganifu; vinamfanya mwanamke kuonekana kuwa mrefu ilihali sio mrefu. Pili vinamtia khatarini mwanamke kuanguka. Tatu vina madhara ya kiafya, jambo ambalo limethibitishwa na madaktari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/397)
  • Imechapishwa: 14/03/2021