Uwajibu wa kumsahihisha imamu anapokosea kisomo

Swali: Ni zipi sharti za kumrekebisha imamu anapokosea katika kisomo chake ndani ya swalah pamoja na kuzingatia kwamba wapo maimamu ambao hawakusubiri na wanarudi kisomo upya?

Jibu: Kumrekebisha imamu ndani ya swalah ni jambo la wajibu. Ni mamoja katika al-Faatihah au Suurah nyingine. Imamu ataposikia anarekebishwa basi ni lazima kwake kurudi katika usawa. Baadhi ya maimamu wanasema kwamba wanaporekebishwa na watu basi wanachanganyikiwa na wanashindwa kuendelea kisomo. Dawa ya hili ni nyepesi; arukuu na akisharukuu hakuna neno. Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma katika swalah ya Fajr Suurah “al-Mu´mimuun” na alipofika katika kisa cha Muusa na Haaruun akatatizika kidogo ambapo akasimama na akarukuu. Vivyo hivyo imamu akichanganyikiwa na mambo basi arukuu. Kila ugonjwa una dawa yake na himdi zote anastahiki Allaah. Ama kuwaambia waswaliji wasikusahihishe ni kosa. Akirekebishwa basi ni lazima asahihishe kwa sababu Qur-aan ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall). Ni lazima asome kama ilivyoteremshwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1146
  • Imechapishwa: 20/06/2019