Uwajibu wa kumfundisha mtu dini yake baada ya kumsilimisha


Swali: Mimi ni katika watu wa misitu kutoka Afrika. Huwalingania watu katika Uislamu lakini sina elimu ya kutosha. Namlingania mtu na kumwambia “Sema: “laa ilaaha illa Allaah” kisha namwacha. Je, mimi nakuwa ni mwenye kupata madhambi kwa hilo?

Jibu: Unapata ujira kwa hili. Mlinganie kwa kiasi cha uwezo wako na elimu yako. Walinganie katika hili na usimwache hivo hivo, mletee makala kadhaa, vitabu kwa lugha yao. Usimwambie tu “Sema: “laa ilaaha illa Allaah” kisha ukamwacha hivo hivo na kwenda zako. Mletee “kijitabu kuhusu Tawhiyd, ´Aqiydah na maana ya laa ilaaha illa Allaah” kwa lugha yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-06.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014