Uwajibu wa kuacha ribaa baada ya kutubia

Swali: Mwenye kuchukua mkopo wa ribaa kutoka benki kwa ajili ya kununua nyumba kisha baadaye akatubia anaguswa na Aayah hii:

وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ

“Mkitubu basi mtapata rasilimali zenu”?

Jibu: Hapana. Huyu ni yule aliyekusanya pesa ya ribaa kisha akatubia kwa Allaah (´Azza wa Jall). Ametubia kwa Allaah baada ya kwamba ana madeni kwa watu ya ribaa.

وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ

“Mkitubu basi mtapata rasilimali zenu.” (02:279)

Katika hali hii anatakiwa kuacha zile faida na achukue rasilimali yake. Achukue rasilimali yake na aache zile faida za ribaa:

وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ

“Mkitubu basi mtapata rasilimali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (63) http://alfawzan.af.org.sa/node/16495
  • Imechapishwa: 26/08/2017