Utani na mzaha katika Uislamu


Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya utani katika dini ya Uislamu? Je, ni jambo linaingia katika maneno ya upuuzi pamoja na kuzingatia kwamba haihusiani na kuchezea dini shere?

Jibu: Hapana vibaya kufanya utani kwa maneno muda wa kuwa ni kwa haki na ukweli khaswakhaswa ikiwa mtu hafanyi hivo kwa wingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya mzaha na hasemi isipokuwa ukweli mtupu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini haijuzu ikiwa ni utani wa wongo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ole wa yule mwenye kuzungumza akadanganya ili awachekeshe watu! Ole wake! Kisha ole wake!”

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/391)
  • Imechapishwa: 07/03/2021