Ususaji kwa ajili ya Allaah hauna muda maalum


Swali: Ni ipi maana ya Hadiyth hii: “Si halali kwa muislamu kumkata ndugu yake zaidi ya siku tatu.”? Inahusu wanandugu? Je, ndugu wa mke wanazingatiwa kuwa ni ndugu?

Jibu: Hadiyth ni yenye kuenea na inahusu wanandugu na wengineo. Haijuzu kwa muislamu kumsusa ndugu yake muislamu sawa akiwa ni ndugu au si ndugu. Lakini ndugu ni kubaya zaidi kwa kuwa ususaji ina maana ya kukata udugu. Haijuzu kumkata ndugu yako kwa sababu tu ya kufahamiana vibaya katika jambo la kidunia. Ikiwa unaona kuwa ni lazima ufanye hivo basi iwe kwa siku tatu. Vinginevyo lililo bora zaidi ni kutomkata kabisa.

Lakini ikiwa ususaji ni kwa ajili ya dini au maasi, ususaji unaendelea mpaka pale atapotubia na sio siku tatu tu. Amkate mpaka pale atapotubu kwa maasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2018