Usiweki pesa benki ila kwa dharurah

Swali 17: Ni hukumu ya mwenye kuweka pesa zake kwenye benki na baadaye wanampa faida? Wako ambao wanaipokea na wako wengine wanaiacha kwa ajili ya benki.

Jibu: Lililo la wajibu ni kuiacha yote kwenye benki. Hakuna kitu chochote kinacholingana na usalama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah basi Allaah atambadilishia bora kuliko hicho.”

Akiipokea basi ameiweka nafsi yake mwenyewe katika laana:

“Allaah amemlaani mwenye kula ribaa, mwenye kuitoa, katibu wake na mwenye kuishuhudia.”

Tumeshatangulia kusema kuwa mtu asiweke pesa zake benki isipokuwa yule anayekhofia pesa zake kuibiwa au kuharibika. Ikiwa mtu hachelei mambo hayo basi haitakikani kuweka pesa zake benki. Kwa sababu anawasaidia kuzitumia pesa hizi na kuchukua faida zake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 64
  • Imechapishwa: 23/10/2019