Usiliache jitu Hizbiy lizungumze msikitini kwako


Kuna imamu msikitini. Amejiwa na Hizbiy na anamuomba aweze kuongea msikitini kwake. Ana uwezo wa kumzuia pasi na kutokea madhara yoyote. Je, amwache aweze kuzungumza halafu baada ya hapo aweke taaliki maneno yake au kuanzia mwanzo amzuie moja kwa moja?

Moja kwa moja. Mambo yanatakiwa kuwa namna hii. Aizuie shari kuanzia mwanzo. Usijiaminishe kwa mtu Hizbiy au mtu wa Bid´ah. Hawastahiki kusikilizwa. Midhali wewe ndiye msimamizi wa msikiti mzuie. Anza kwanza kwa kujirekebisha mwenyewe. Cha kwanza anatakiwa kujirekebisha mwenyewe. Je, mmenisikia mimi nikisema kitu kingine? Je, mmenisikia mimi nikisema kwamba azungumze halafu baada ya hapo yafanyiwe taaliki? Hapana. Maneno yetu yako imara na tunamuomba Allaah atuthibitishe katika Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-14107
  • Imechapishwa: 19/09/2020