Usiku wa Qadr ni katika Ramadhaan

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ

“Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-aan katika usiku wa Qadr.”

Hakuna kipingamizi kwamba kinacholengwa ni ushushwaji wa Qur-aan tukufu. Allaah (Ta´ala) ameiteremsha katika usiku wa Qadr. Nini maana kwamba Qur-aan imeteremshwa katika usiku wa Qadr? Sahihi ni kwamba imeanza kuteremshwa katika usiku wa Qadr. Hapana shaka kuwa usiku wa Qadr unakuwa katika Ramadhaan. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ

“Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan.”

Zinapooanishwa Aayah hizi mbili basi inapata kubainika kuwa usiku wa Qadr unatokea katika Ramadhaan. Kwa haya tunapata kujua kwamba yale yaliyotangaa kwa watu wasiokuwa na elimu eti usiku wa Qadr unatokea katika usiku wa nusu Sha´baan ni jambo lisilokuwa na msingi wala ukweli wowote. Hakika usiku wa Qadr unatokea katika Ramadhaan na usiku wa nusu Sha´baan ni kama nyusiku za miezi mingine yote ya mwaka; haunasibishiwi ´ibaadah yoyote maalum.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 272-273
  • Imechapishwa: 14/05/2020