Usiku wa Qadr kwa mujibu wa Ubayy bin Ka´b

793- Waaswil bin ´Abdil-A´laa al-Kuufiy ametuhadithia: Abu Bakr bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim, kutoka kwa Zirr aliyesema:

“Umejuaje, ee Abul-Mundhir, kwamba usiku wa Qadr ni usiku wa tarehe ishirini na saba?” Akasema: “Ndio. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametueleza alama ya usiku huo ni kwamba jua siku hiyo linachomoza asubuhi likiwa halina miale ya kuchoma. Tukahesabu na kuhifadhi. Ninaapa kwa Allaah! Ibn Mas´uud alijua kuwa unatokea katika Ramadhaan na kwamba ni usiku wa tarehe ishirini na saba, lakini amechukia kukwambie mkaja kubweteka.”[1]

Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (793).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Iysaa Muhammad bin ´Iysaa at-Tirmidhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jaami´ (793)
  • Imechapishwa: 15/05/2020