Swali: Inafaa kwa mnaswara akawa shahidi katika ndoa?

Jibu: Hapana. Waislamu hawatakiwi kuwatumia makafiri kama mashahidi. Isipokuwa tu wakati wa wasia endapo hakutopatikana ushahidi wa muislamu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ

“Enyi mlioamini! Ushahidi [uweko kushuhudiwa] baina yenu yanapohudhuria mauti kwa mmoja wenu wakati anapousia. Waweko mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu au wawili wengine wasiokuwa nyinyi [makafiri] mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya swalah na waape kwa Allaah mkitilia shaka: “Hatutobadilisha kwayo kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.”” (06:165)

Ikiwa hakuna shahidi muislamu atayeshuhudia wasia mnaswara ashuhudie hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017