Usaamah bin Laadin anawakufurisha waislamu


Watu wajinga ndio wataendesha harakati? Ni genge la wajinga katika Jamaa´at-ul-Jihaad au Suruuriyyah ndio wataendesha harakati za Kiislamu? Ni wanachuoni ndio wanatakiwa kuwaongoza:

وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ

”Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye elimu.” (29:43)

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ

“Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale wanaotaka maisha ya dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruun, hakika yeye ana bahati kubwa mno” na Wakasema wale waliopewa elimu: “Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.” (28:79-80)

Ni wajibu kurejea kwa wanachuoni:

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖوَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ

“Linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu basi hulitangaza na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wenye madaraka kati yao, basi wale wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua.” (04:83)

Jamaa´at-ut-Takfiyr ambao wanawakufurisha Waislamu na wanahalalisha damu yao Baydhaa´, San´aa´ na miji mingine, ni wenye kuhitajia Da´wah. Wanahitajia vilevile serikali itaalimiane nao kwa uadilifu, kuwafunga na kuwatuma kwa wanachuoni wajadiliane nao. Jamaa´at-ul-Jihaad na makundi mengine yanayoeneza ufisadi ambayo wakati huo huo mtayapata katika Jamaa´at-ul-Takfiyr.

Usaamah alikuwa anatumai kutoka kwangu nimfanyie kumkufurisha ´Aliy ´Abdullaah Swaalih. Usaamah bin Laadin… hii ni dalili ya kwamba anawakufurisha waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye atamwambia ndugu yake ´ewe kafiri`, basi litamrudi mmoja wao.”

Unapomwambia ndugu yako kwamba ni kafiri, aidha ni kama ulivosema au neno hilo linakurudilia wewe mwenyewe.