Unapolazimika kuwa na picha


Swali: Ni ipi hukumu ya picha ikiwa mtu ametenzwa nguvu juu ya hilo?

Jibu: Dharurah ikipelekea katika picha kama mfano wa mmiliki wa ushirika, leseni na mfano wa hayo nataraji hakuna neno. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.” (06:119)

Ama pasi na dharurah haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watenegeneza picha.”

Jengine yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kula ribaa, wakala wake na amewalaani watengeneza picha. Zipo Hadiyth nyingi juu ya maudhui haya. Zinazokusudiwa ni picha za viumeb wenye roho katika wanadamu na viumbe vyenginevyo.

Kuhusu kuchukua picha viumbe visivyokuwa na roho kama mfano wa miti, milima, magari na vyenginevyo hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/390)
  • Imechapishwa: 01/08/2021